Uharibifu wa mazingira

Zaidi ya miaka themanini baada ya kuondoka katika magodi ya Wallaroo (Kadina, Australia kusini), vigoga vinabakia kama uoto pekee katika eneo hili.

Uharibifu wa mazingira ni uzoroteshaji wa mazingira kwa njia ya kupunguza rasilimali kama vile hewa, maji na udongo na kupotea kwa wanyamapori. Uharibifu wa mazingira ni wa aina nyingi. Wakati ni makazi asili yanaharibiwa au maliasili kutumiwa vibaya, tunasema kuwa mazingira yanaharibiwa.

Uharibifu wa mazingira ni moja ya vitisho kumi vilivyoonywa na jopo la juu la vitisho vikuu la Umoja wa Mataifa. Shirika la raslimali ulimwenguni, Umoja wa Mataifa wa Mpango wa Mazingira, Umoja wa Mataifa wa Maendeleo na Benki ya Dunia zimetoa ripoti kwa umma kuhusu afya na mazingira duniani tarehe 1 Mei 1998.

Mabadiliko ya mazingira na afya ya binadamu, sehemu maalum katika ripoti hiyo inaeleza jinsi magonjwa yana uwezo wa kuzuiwa na vifo vya mapema bado huzidi kuongezeka kwa idadi kubwa. Ikiwa kuna marekebisho makubwa katika afya ya binadamu mamilioni afya ya binadamu, mamilioni ya watu watakuwa wangeishi kwa muda mrefu,na maisha yenye afya nzuri kuliko awali. Katika maeneo maskini katika dunia inakadiriwa kuwa mmoja katika watoto watano hawataishi kuona siku yao ya kuzaliwa ya tano, hasa kwa sababu ya magonjwa yanayohusiana na mazingira. Watoto Milioni kumi na moja duniani kote hufa kila mwaka, sawa na wakazi wa Norway na Uswisi, wakiunganishwa na hasa kutokana na malaria, shida za kupumua au kuhara - magonjwa ambayo yanaweza kukingwa.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search