Uholanzi

Koninkrijk der Nederlanden
Ufalme wa Nchi za Chini
Bendera ya Uholanzi Nembo ya Uholanzi
Bendera Nembo
Hadabu ya Taifa: Je maintiendrai
(Kifaransa)
kwa Kiswahili, Nitastahimili
Mahali pa Uholanzi
Lugha za Taifa
Kiholanzi
kwa mkoa wa Friesland: Kifrisi
Mji Mkuu Amsterdam
Makao ya Serikali Den Haag
Mfalme Koning Willem-Alexander
Waziri Mkuu Mark Rutte
Eneo
 - Jumla
 - % Maji

41,526 km²
18.41
Umma
 - Jumla
 - msongamano

16,856,620 (Julai 2014)
406.4/km²
GDP
 - Jumla
 - kwa kipimo cha umma

$625 bilioni
$ 30,500
Uhuru
 - Tangazwa
 - Kukubaliwa
Kutoka Hispania
  26 Julai 1581
  30 Januari 1648
Fedha Euro € EUR
Saa za Eneo UTC +1
Wimbo wa Taifa Wilhelmus
TLD mtandao .nl
Kodi ya simu 31

Uholanzi ni nchi ya Ulaya ya Magharibi. Imepakana na Ujerumani upande wa mashariki, Ubelgiji upande wa kusini na Bahari ya Kaskazini (North Sea) upande wa magharibi na kaskazini.

Uholanzi ni sehemu ya "Ufalme wa Nchi za Chini" (Kingdom of the Netherlands) pamoja na visiwa vya Aruba, Curaçao na Sint Maarten, mbali ya visiwa vingine vitatu vya Karibi vya Uholanzi.

Jina la Uholanzi limetokana na “Holland”, eneo la magharibi la nchi hii. Watu wengi hutumia jina hilo, lakini wakazi wenyewe wanaiita nchi yao “Nederland” inayomaanisha "nchi ya chini". Kwa kweli, sehemu kubwa ya Uholanzi iko chini ya usawa wa bahari. Waholanzi wamejenga maboma kuzuia maji yasienee yakifurika.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search