Umoja wa Mataifa

Nchi wanachama      193 yanachama ya UM      2 yaangalizi ya UM (Mji wa Vatican, Jimbo la Palestina)      2 yasiyo yanachama yanayostahiki (Visiwa vya Cook, Niue)      maeneo 17 yasiyo ya kujitawala      1 eneo la kimataifa (Antaktika)

Umoja wa Mataifa (UM) (Kiingereza: United Nations, UN) ni shirika la kiserikali ambalo malengo yake ni kudumisha amani na usalama wa kimataifa, kuendeleza uhusiano wa kirafiki kati ya mataifa, kufikia ushirikiano wa kimataifa, na kuwa kituo cha kuoanisha matendo ya mataifa. Ni umoja wa nchi zote duniani isipokuwa zile zisizotambuliwa kuwa dola huru.

Umoja huo ulianzishwa na nchi washindi wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia kuchukua nafasi ya Shirikisho la Mataifa (1919 - 1946). Makubaliano yalifikiwa tarehe 24 Oktoba 1945 huko San Francisco, California.

Mwanzoni nchi zilikuwa 51 lakini kufikia mwaka 2017 kulikuwa na nchi wanachama 193, mbali ya Ukulu mtakatifu (Vatikani) na Palestina ambazo zinashiriki kama watazamaji wa kudumu, zikiwa na haki karibu zote isipokuwa kupiga kura.

Dhumuni la umoja huu ni kuratibu mahusiano ya kimataifa kupitia sheria na mikataba ya kimataifa kwenye maeneo kama usalama, amani, maendeleo ya jamii na ya uchumi, haki za binadamu, uhuru, demokrasia n.k.

Toka mwanzo makao makuu ya Umoja wa Mataifa yako Manhattan, New York City, New York nchini Marekani na hayako chini ya mamlaka ya nchi hiyo. Ofisi nyingine ziko Geneva (Uswisi), Nairobi (Kenya) na Vienna (Austria).

Lugha rasmi za UM ni sita: Kiarabu, Kichina, Kifaransa, Kihispania, Kiingereza na Kirusi.

Katibu Mkuu wa UM anachaguliwa kwa miaka mitano; kwa sasa ni António Guterres kutoka Ureno, aliyechaguliwa kuwa Katibu Mkuu mwaka 2016 akichukua nafasi ya Ban Ki-moon.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search