Visiwa vya Mariana

Visiwa vya Mariana (kwa Kiingereza: Mariana Islands) ni funguvisiwa la Pasifiki ya magharibi, takriban katikati ya Papua Guinea Mpya na Japani. Vinahesabiwa kati ya visiwa vya Melanesia.

Kwa jumla ni safu ya visiwa 15 vyenye asili ya volkeno kati ya 12 hadi 21N na mnamo 145E.

Vyote ni maeneo ya ng'ambo ya Marekani inayotawala funguvisiwa hilo kama vitengo viwili vya pekee:

  • Visiwa vya Mariana ya Kaskazini (Northern Mariana Islands) ambavyo ni idadi kubwa ya visiwa hivyo na eneo lenye madaraka ya kujitawala
  • Guam ambayo ni kisiwa kikubwa pekee ambacho ni kituo cha kijeshi cha Marekani.

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search