Wazazi

Sanamu ya wazazi wawili na mtoto wao huko Bratislava, Slovakia.

Wazazi ni wale waliofanya watoto wapatikane katika spishi yao.

Kwa wanadamu, mzazi ndiye mlezi wa mtoto. Inafaa sana uzazi uendelezwe na malezi hadi kumfanya mtoto akomae pande zote na kuwa mtu mzima, tena bora.

Mzazi wa kibiolojia ni mtu ambaye gamete yake imetoa mtoto, mzazi wa kiume kupitia manii, na mwanamke kupitia kijiyai. Wazazi hao, baba na mama, ni jamaa ya kwanza na kuchangia asilimia 50 ya maumbile ya mtoto.

Mwanamke, mbali ya kujifungua, anaweza kuwa mzazi kwa njia ya upasuaji pia, hasa pale ambapo ujauzito una matatizo .

Siku hizi inawezekana kuwa na wazazi wa kibiolojia zaidi ya wawili, pale ambapo mtoto anatengenezwa katika maabara. Jambo hilo linapohusu binadamu, wengine wanalipinga kwa kusema ni kinyume cha maumbile na cha hadhi ya utu, pamoja na kudai mimba nyingi ziangamie au kutunzwa katika jokofu.

Wazazi wengine wanaweza kuwa wazazi kwa kukubaliana, ambao huwalea watoto, lakini si kweli kwamba wanahusiana na mtoto kimaumbile.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search