Kibalantak

Kibalantak (pia Kikosian) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wabalantak kwenye kisiwa cha Sulawesi. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kibalantak imehesabiwa kuwa watu 30,000. Pia wasemaji wa lugha jirani hujifunza Kibalantak kama lugha ya mawasiliano. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibalantak iko katika kundi la Kicelebiki.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search