Kibanggai

Kibanggai (pia Kiaki) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wabanggai kwenye visiwa vya Banggai. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kibanggai imehesabiwa kuwa watu 125,000. Hata hivyo Kibanggai imeanza kutoweka kwa vile Wabanggai wengi wameanza kuacha lugha yao. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibanggai iko katika kundi la Kicelebiki.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search