Kitai-Yo (pia Kitai-Do) ni lugha ya Kitai-Kadai nchini Vietnam na Laos inayozungumzwa na Watai. Mwaka wa 2002 idadi ya wasemaji wa Kitai-Yo nchini Vietnam imehesabiwa kuwa watu 300 tu. Pia kuna wasemaji 7200 nchini Laos (1995) ambao hudai kwamba wametoka nchi ya Vietnam kiasili. Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kitai-Yo iko katika kundi la Kitai ya Kaskazini.
© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search