Waidakho

Waidakho ni miongoni mwa makundi madogo ya kabila la Abaluhya wanaokalia eneo la rutuba nyingi la Kaunti ya Kakamega, Magharibi mwa Kenya. Eneo wanalokalia Waidakho linajulikana kiutawala kama Ikolomani, ambalo ndilo jimbo la uchaguzi pekee katika eneo hili, mji mkuu wake ukiwa Malinya. Mbunge wa sasa ni Bonny Khalwale.

Kama ilivyo na kawaida katika maeneo ya Kenya Magharibi, eneo la Idakho lina wingi wa wakazi huku makadirio ya idadi ya wakazi mwaka wa 2007 yakiwa yamezidi watu 150,000.

Upungufu wa mashamba na utandawazi vimewalazimu Waidakho kubadili mtindo wao wa maisha huku wengi wakijihusisha na ukulima wa ng'ombe wa maziwa na kwa kiwango kidogo, ukulima wa majani ya chai. Mhindi hata hivyo ndio mmea unaokuzwa zaidi, ukiwapa chakula chao cha kawaida - sima (ubushuma). Huvunwa mara mbili kwa mwaka.

Hata hivyo, hali yao ya kimaisha ya kiutamaduni huwasaidia tu kuishi maisha yao ya kisasa.

Wengi wao wakiwa na kiwango fulani cha masomo (62%), Waidakho siku hizi wanajiusisha kwenye sekta za biashara, wafanyakazi wa umma na sekta za binafsi kwenye miji mikuu ya Afrika Mashariki.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search