Afya

Stempu ya posta ya New Zealand, mnamo mwaka 1933.
Mwanamke akinawa mikono 1655 hivi.
Donald Henderson na wenzake katika kukinga watu dhidi ya ndui mwaka 1966.

Afya ni hali ya kujisikia vizuri kimwili, kiakili, kiroho na kiutu bila kusumbuliwa na ugonjwa wowote.

Afya ya binadamu itakuwa njema kama atafuatilia kanuni na taratibu bora za afya. Hiyo inajumuisha mlo kamili, yaani chakula chenye virutubishi vyote, vikiwemo protini, wanga na mafuta (hiyo iwe katika asilimia ndogo sana).

Pia anatakiwa awe msafi mwilini na mazingira yake, kama vile kwa kuoga na kusafisha mazingira yanayomzunguka. Mandhari yenye hewa safi pia husaidia katika kuhifadhi afya ya binadamu katika mwili na akili.

Mazingira mara nyingi huchukuliwa kuwa jambo muhimu katika hali ya afya ya binadamu. Hii inajumuisha mazingira ya asili, mazingira ya kujengwa, na mazingira ya kijamii. Pia mambo kama vile maji safi na hewa, makazi salama, huchangia afya nzuri, hasa kwa afya ya watoto wachanga na watoto.[1]

Utafiti umeonyesha kuwa ukosefu wa maeneo ya burudani husabsabisha kupungua kwa afya na ustawi.[2]


Pia anatakiwa kuwa na afya ya kiroho yaani kuishi kadiri ya mafundisho ya Mwenyezi Mungu kama vile: kupendana na wengine, kuthaminiana na kuacha dhambi: mara nyingi hizo zinadhuru afya ya mwili pia.

  1. http://www.who.int/hia/evidence/doh/en/
  2. "Faida za maeneo ya burudani kwenye afya".

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search