California








California

Bendera

Nembo
Nchi Bendera ya Marekani Marekani
Mji mkuu Sacramento
Eneo
 - Jumla 423,970 km²
 - Kavu 403,933 km² 
 - Maji 20,037 km² 
Tovuti:  http://www.ca.gov/

California (pia: Kalifornia) ni jimbo la Marekani upande wa magharibi-kusini ya nchi. Iko kwenye pwani ya Pasifiki ikipakana na Meksiko (Baja California).

Wakazi wamekadiriwa kuwa 39,512,223 mwaka 2019.

California ni kati ya majimbo ya Marekani yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi. Kama California ingekuwa nchi huru ya kujitegemea uchumi wake ungekuwa na nafasi ya 8 duniani. Utalii, kilimo na viwanda vya ndege huajiri watu wengi. Kampuni za kompyuta zimestawi vizuri sana California, kwa mfano Microsoft. Los Angeles, hasa eneo la Hollywood, ni kitovu cha kupiga picha za filamu.

Mji mkuu ni Sacramento. Kuna miji 59 yenye wakazi zaidi ya lakhi moja:

Mji Wakazi
1 Los Angeles 3.957.875
2 San Diego 1.305.736
3 San Jose 944.857
4 San Francisco 799.263
5 Fresno 500,017
6 Long Beach 491.564
7 Sacramento 452.959
8 Oakland 412.318
9 Santa Ana 351.697
10 Anaheim 345.317
Hifadhi ya Redwood
Mlima Shasta
Yosemite National Park

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search