Chawa | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Chawa wa kichwa (Pediculus humanus capitis)
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Familia za juu 4: |
Chawa ni wadudu wadogo wa oda ndogo Phthiraptera katika nusuoda Troctomorpha wa oda Psocodea. Wahenga wao ni chawa-vitabu na kama hawa chawa hawana mabawa. Wadudu hawa wote ni vidusia wa nje juu ya ndege na mamalia isipokuwa Monotremata (kinyamadege na mhanganungu), popo, nyangumi, pomboo na kakakuona. Kuna aina mbili za chawa: wanaokula nywele, manyoya na seli za ngozi zilizokufa, na wanaofyunza damu ya mwenyeji. Chawa wa aina ya kwanza wana vipande vya mdomo vya kutafuna, wale wengine wana mdomo wa kufyunza. Miguu inabeba aina za magando madogo ili kushika nywele au manyoya ya mwenyeji. Kwa kawaida mayai ya chawa yamegandia nywele au manyoya, au pengine yamewekwa ndani ya shina la unyoya.
Binadamu ni kidusiwa wa spishi mbili: chawa wa binadamu (Pediculus humanus) na chawa-kinenani (Pthirus pubis). P. humanus imegawanya katika nususpishi mbili kufuatana na sehemu ya mwili ambapo zinakaa: chawa-kichwani (P. h. capitis) na chawa-mwilini (P. h. humanus). Chawa wa binadamu wana uhusiano wa karibu na chawa wanaopatikana kwenye sokwe mtu wa kawaida na bonobo, hata hivyo chawa-kinena wako karibu zaidi na chawa wa ngagi. Ingawa chawa wa binadamu wanafikiriwa kuwa waligeua tangu wanadamu watengane na sokwe mtu, chawa-kinenani wanaonekana kuwa waliambukiza wanadamu katika hatua za baadaye za mageuzi yao, yumkini wakati wa kulala kwenye viota vya ngagi au wakati wa kuwachinja, na kutengana na chawa wa ngagi.
© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search