Fedha (kutoka Kiarabu فضة fiddtan) ni elementi na metali yenye kifupi cha Ag (kutoka Kilatini: argentum) na namba atomia 47 katika mfumo radidia. Uzani atomia ni 107.86. Fedha huyeyuka kwa 1234.93 K (961.78°C) na kuchemka kwa 2435 K (2162°C).
Kiasili yatokea kama metali nyeupenyeupe na laini au kama mchanganyiko katika madini. Kati ya metali zote fedha ni wayaikaji na inapitisha vizuri umeme.
© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search