Gedi


Gede
Nchi Kenya
Kaunti Kilifi
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 600
Maghofu ya msikiti
Kaburi la mwaka 1399 kati ya maghofu ya Gedi

Gedi (pia: Gede) ni kijiji cha wakazi 600 kwenye pwani ya Kenya kusini mashariki katika Kaunti ya Kilifi, takriban kilomita 16 kusini kwa Malindi. Ni mahali maarufu pa maghofu ya mji wa Waswahili wa Kale ndani ya msitu wa Arabuko-sokole.[1]

Kuna maeneo 116 ya Waswahili yanayonyooka kutoka kusini mwa Somalia mpaka Vumba kuu katika mpaka wa Kenya na Tanzania.[2] kutokana na uvumbuzi wa magofu ya Gedi uliofanywa na wakoloni miaka ya 1920, Gede imejulikana kama mji uliotambulika zaidi na maeneo yake kufanyiwa utafiti zaidi kando na maeneo ya Shanga, Manda, Ungwana, Kilwa na visiwa vya Komoro.

  1. https://web.archive.org/web/20161202145130/http://www.museums.or.ke/content/blogcategory/22/28/
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-06-16. Iliwekwa mnamo 2022-08-12.

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search