George mfiadini

Mchoro wa Hans von Kulmbach (1510 hivi).
Mt. George akiua joka (De Grey Hours, 1400 hivi)
Picha takatifu wa Urusi (karne ya 14), Novgorod.
Mchoro mdogo wa karne ya 13 katika kitabu Passio Sancti Georgii (Verona, Italia).

George (kwa Kigiriki: Γεώργιος, Geṓrgios, yaani Mkulima; kwa Kilatini: Georgius; 256/285 - 23 Aprili 303) alikuwa askari wa Dola la Roma ambaye inasemekana alifanya kazi kama afisa katika kikosi cha kumlinda kaisari Diocletian[1].

Huyo alipoanza dhuluma dhidi ya Wakristo, Joji alikataa kuasi imani yake, akauawa huko Lydda (leo nchini Israeli)[2].

Tangu kale anaheshimiwa sana na Wakristo wa madhehebu mengi kama mtakatifu[3].

Hata katika vitabu vya Uislamu anatajwa kama nabii جرجس, Jiriyas (au Girgus)[4].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 23 Aprili, siku ya kifodini chake[5].

  1. Attwater, Donald (1995) [1965]. Dictionary of Saints (toleo la Third). London: Penguin Reference. uk. 152. His best-known story, popularized in the later middle ages by the Golden Legend, tells that he was a knight from Cappadocia, who rescued a maiden princess from a dragon at Silene in Libya, leading to the Christianity of much of the kingdom.
  2. http://www.santiebeati.it/dettaglio/26860
  3. George Mtakatifu ametajwa katika Kitabu cha Sala ya Kawaida (kwa Kiingereza Book of Common Prayer) wa mwaka 1662, na pia katika Kitabu cha Ibada ya Kawaida (kwa Kiingereza Common Worship) mwaka wa 2000. Hata hivyo, makanisa mengine ya Kianglikana hawamtambui kama mtakatifu.
  4. Scott B. Noegel, Brannon M. Wheeler. The A to Z of Prophets in Islam and Judaism. Rowman & Littlefield. uk. 313.
  5. Martyrologium Romanum

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search