Ghuba ya Carpentaria

Mahali pa Ghuba ya Carpentaria.
Ghuba ya Carpentaria katika ramani ya Kiholanzi ya mwaka 1859.

Ghuba ya Carpentaria (14°00′S 139°00′E / 14.000°S 139.000°E / -14.000; 139.000) ni sehemu ya bahari kwenye kaskazini ya Australia. Pande za kusini, magharibi na mashariki iko Australia bara, upande wa kaskazini iko Bahari iliyopo baina ya Australia na Guinea Mpya. Kwenye kinywa chake, ghuba ina upana wa km 590, urefu wa kaskazini hadi kusini ni km 700.

Eneo la maji ni takribani km² 300,000. Maji yake huwa na kina kati ya mita 55 hadi 66, ingawa kuna sehemu zenye mita 82. [1]

  1. http://permanent.access.gpo.gov/websites/pollux/pollux.nss.nima.mil/NAV_PUBS/SD/pub175/175sec01.pdf

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search