Historia ya Kosovo

Historia ya Kosovo inahusu eneo ambalo leo linaunda jamhuri ya Kosovo.

Kihistoria Kosovo iliwahi kuwa eneo ambako ufalme wa kwanza wa Serbia ulianzishwa wakati wa karne ya 12. Hivyo Kosovo ilikuwa kitovu cha Serbia hadi mwisho wa milki ya Serbia ya Kale iliyovamiwa na Waturuki wa Milki ya Osmani.

Chini ya utawala wa Waturuki idadi ya Waserbia ilipungua kwa sababu wengi walikimbia ukandamizi wa Waosmani dhidi ya Wakristo. Waalbania walihamia humo kutoka maeneo ya jirani yaliyokuwa pia sehemu ya Milki ya Osmani. Katika karne ya 19 idadi kubwa ya wakazi wa Kosovo walikuwa tayari Waalbania.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search