Ignas wa Antiokia

Kifodini cha Mt. Ignas.

Ignas wa Antiokia (kwa Kigiriki Ἰγνάτιος, Ignatios: lakini alijulikana pia kwa jina la Θεοφόρος, Theophoros, yaani "Mleta Mungu") alizaliwa kati ya miaka 35 na 50 B.K. akafa kati ya 98 na 117.[1]

Ni kati ya Mababu wa Kanisa wa kwanza, akiwa mwanafunzi wa Mitume wa Yesu na askofu wa tatu wa Antiokia, leo nchini Uturuki.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake inaadhimishwa na Wakatoliki[2][3], Waanglikana na Waorthodoksi wa Mashariki kwenye 17 Oktoba, lakini na Waorthodoksi tarehe 20 Desemba.

  1. Tazama: "Ignatius" katika The Westminster Dictionary of Church History, ed. Jerald Brauer (Philadelphia:Westminster, 1971) na pia David Hugh Farmer, "Ignatius of Antioch" katika The Oxford Dictionary of the Saints (New York: Oxford University Press, 1987).
  2. Calendarium Romanum (Vatican City, 1969)
  3. Martyrologium Romanum

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search