Jangwa la Gobi

Ramani ya jangwa la Gobi.

Jangwa la Gobi (kwa Kiingereza: Gobi Desert; kwa lugha ya Mandarin linaitwa Gobi, 戈壁, yaani brushland) ni jangwa kubwa la Asia[1] likienea kwa kilomita mraba 1,295,000[2].

Linaenea kaskazini mwa China na kusini mwa Mongolia, kusini kwa milima ya Altai.

Sababu yake ni kwamba nyanda za juu za Tibet huzuia mvua kutoka Bahari ya Hindi zisifike hadi Gobi.

Katika historia ni maarufu kama sehemu ya Dola la Mongolia na mahali pa miji muhimu ya Silk Road.

  1. Sternberg, Troy; Rueff, Henri; Middleton, Nick (2015-01-26). "Contraction of the Gobi Desert, 2000–2012". Remote Sensing (kwa Kiingereza). 7 (2): 1346–1358. doi:10.3390/rs70201346.{{cite journal}}: CS1 maint: unflagged free DOI (link)
  2. Wright, John W., mhr. (2006). The New York Times Almanac (toleo la 2007). New York, New York: Penguin Books. uk. 456. ISBN 978-0-14-303820-7.

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search