| |
Rais wa Tanzania | |
Tarehe ya kuzaliwa | 29 Oktoba 1959 |
Tarehe ya kifo | 17 Machi 2021 |
Chama | CCM |
Dini | Ukristo (Kanisa Katoliki) |
Elimu yake | Mwanakemia |
Digrii anazoshika | Shahada ya Uzamivu |
Kazi | Mwanasiasa |
John Pombe Joseph Magufuli (29 Oktoba 1959 - 17 Machi 2021) alikuwa rais wa tano wa Tanzania, akitokea katika chama cha Mapinduzi CCM. Aliongoza kwa muda wa miaka mitano na nusu hadi kifo chake[1].
Aliwahi kuwa Mbunge wa jimbo la Biharamulo Mashariki katika bunge la kitaifa huko nchini Tanzania na tangu mwaka 2010 aliteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi.[2]
Tarehe 12 Julai 2015 alichaguliwa kuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi akiwa na mgombea mwenza Samia Suluhu Hassan.
Tarehe 29 Oktoba 2015 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilimtangaza kuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushindi wa kura 8,882,935 sawa na 58.46% pamoja na makamu wa rais Samia Suluhu Hassani.
Tarehe 5 Novemba 2015 aliapishwa kama rais wa tano wa Tanzania, ingawa upinzani haukukubali matokeo hayo.
Baada ya uchaguzi wa tarehe 28 Oktoba 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilimtangaza tena mshindi pamoja na makamu wa rais Samia Suluhu Hassan kwa kura 12,516,252 sawa na 84.4% ingawa kulikuwa na malalamiko makubwa[3].
© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search