Kalenda ya Kiajemi

Mkataba wa Irani uliochapishwa mwaka 1910,ukiwa unafuata kalenda ya Hijra.

Kalenda ya Kiajemi ni kalenda rasmi katika nchi za Iran na Afghanistan. Ni kalenda ya jua yenye siku 365 na siku 366 katika mwaka mrefu. Mwaka hugawiwa kwa miezi 12.

Mwaka unaanza kwenye 1 Farwardin ambayo ni sawa na 21 Machi, isipokuwa katika mwaka mrefu wa Kalenda ya Gregori ni 20 Machi.

Hesabu ya miaka unafuata hijra ya Mtume Muhamad, kwa hiyo hesabu inaanza katika mwaka 622 ya kalenda ya Gregori. Mwaka 2014 wa kimataifa unalingana na miaka 1392/1393 wa kalenda ya Kiajemi.

Kalenda hiyo inatumiwa pamoja na kalenda ya Kiislamu inayoanza hesabu yake pia kwenye Hijra lakini kwa sababu ni kalenda ya mwezi miaka yake ni mifupi, hivyo mwaka 1393 wa Kiajemi unalingana na mwaka 1435 wa Kiislamu. Ilhali hesabu zote mbili zina msingi wa Kiislamu kwa kurejea hijra zinatofautishwa pia kwa kutumia majina "hijri shamsi" (hijri ya jua) na "hijri qamari" (hijri ya mwezi).


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search