Kanisa kuu la Roma

Upande wa mbele wa Basilika kuu la Mt. Yohane huko Laterano wakati wa usiku. Juu ya paa, pamoja na sanamu ya Yesu Mkombozi na wengine, zipo 12 za Mitume wa Yesu.

Kanisa kuu la Roma ni jengo la ibada lililopo tangu karne ya 4 hadi leo katika mtaa wa Laterani mjini Roma.

Ni kwamba, kama majimbo yote ya Kanisa Katoliki, jimbo la Roma, ambalo askofu wake ni mkuu wa maaskofu wote, lina jengo moja la ibada linaloheshimiwa kama ishara ya umoja wa waamini wake.

Likiwa kanisa kuu la Papa, papo hapo ni kanisa kuu la dunia nzima kwa Wakristo wenye ushirika kamili naye.

Kanisa hilo liliwekwa wakfu mwaka 314 kwa heshima ya Kristo Mkombozi, lakini linajulikana zaidi kwa jina la Mt. Yohane (Mbatizaji), msimamizi wa Roma.

Sikukuu ya kutabaruku kanisa hilo inaadhimishwa na Wakatoliki tarehe 9 Novemba[1]

  1. Martyrologium Romanum

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search