Kanisa la Roma

Ukulu mtakatifu wa Papa katika Kanisa kuu la Roma.
Batizio (kulia) na Jumba la Laterano, makao makuu ya jimbo (kushoto).

Kanisa la Roma ni hasa jimbo la Kanisa Katoliki lilipo katika mji wa Roma (Italia) na kandokando yake.

Ukristo ulifikia huko mwaka uleule wa kifo na ufufuko wa Yesu (kadiri ya imani ya wafuasi wake) unaodhaniwa kuwa 30 BK.

Kadiri ya Matendo ya Mitume sura ya 2, baadhi ya watu ambao siku ya Pentekoste ya mwaka huo walisikilizwa hotuba za Mtume Petro na wenzake wakabatizwa walikuwa wametokea Roma.

Baadaye Mtume Paulo aliliandikia barua yake ndefu kuliko zote, na hatimaye alifanya utume wake huko kwa miaka kadhaa, hata alipouawa (64-67) katika dhuluma ya Kaisari Nero iliyomuua pia Petro huko Vatikani.

Kutokana na kifodini hicho, Wakatoliki wanasadiki Kanisa la Roma limeachiwa mamlaka ya mkuu wa mitume, hivi kwamba askofu wa Roma (yaani Papa) ni mkuu wa maaskofu wote duniani.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search