Katerina wa Aleksandria

Mt. Katerina alivyochorwa na Bernardino Luini (National Art Museum of Azerbaijan).
Mchoro wa Artemisia Gentileschi.
Mchoro wa Carlo Crivelli.
Picha takatifu ya Mt. Katerina wa Aleksandria, na vituko vya kifodini chake.

Katerina wa Aleksandria (kwa Kigiriki ἡ Ἁγία Αἰκατερίνα ἡ Μεγαλομάρτυς; 282-305 hivi) alikuwa bikira Mkristo wa Aleksandria, Misri ambaye aliuawa kwa amri ya kaisari Maxentius mwanzoni mwa karne ya 4[1].

Kadiri ya mapokeo, alikuwa wa ukoo maarufu[2] tena msomi. Kisha kuongokea Ukristo akiwa na umri wa miaka 14, aliongoza watu mia kadhaa kumfuata katika dini hiyo[3].

Tangu alipofia dini anaheshimiwa na Wakristo wa madhehebu mbalimbali kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 24 Novemba au 25 Novemba.[4][5][6]

  1. "Clugnet, Léon. "St. Catherine of Alexandria." The Catholic Encyclopedia. Vol. 3. New York: Robert Appleton Company, 1908. 1 May 2013". Newadvent.org. 1908-11-01. Iliwekwa mnamo 2013-08-26.
  2. "Great Martyr Catherine of Alexandria".
  3. "Saint Catherine of Alexandria". Encyclopædia Britannica. Iliwekwa mnamo 2010-10-29.
  4. Calendarium Romanum (Libreria Editrice Vaticana, 1969), p. 147
  5. Martyrologium Romanum (Libreria Editrice Vaticana, 2001 ISBN 88-209-7210-7)
  6. http://catholicsaints.info/saint-catherine-of-alexandria/

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search