Kaunti ya Kilifi

Kaunti ya Kilifi
Kaunti
Bendera Nembo ya Serikali
Kilifi County in Kenya.svg
Kaunti ya Kilifi katika Kenya
Nchi Kenya
Namba3
IlianzishwaTarehe 4 Machi, 2013
Ilitanguliwa naMkoa wa Pwani
Makao MakuuKilifi
Miji mingineMalindi
GavanaAmason Jefa Kingi
Naibu wa GavanaGideon Edmund Saburi
SenetaStewart Mwachiru Shadrach Madzayo
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa)Getrude Mbeyu Mwanyanje
Bunge la KauntiBunge la Kaunti ya Kilifi
SpikaJimmy Kahindi
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa35
Maeneo bunge/Kaunti ndogo7
Eneokm2 12 539.7 (sq mi 4 841.6)
Idadi ya watu1,453,787
Wiani wa idadi ya watu116
Kanda mudaSaa za Afrika Mashariki (UTC+3)
Tovutikilifi.go.ke

Kaunti ya Kilifi ni kaunti nchini Kenya katika eneo la Mkoa wa Pwani wa awali. Ilianzishwa mwaka 2010 kwa kuunganisha wilaya za Kilifi na Malindi.

Eneo lake ni km² 12,539.7. Eneo hilo lilikuwa na wakazi 1,453,787 wakati wa sensa ya mwaka 2019, msongamano ukiwa hivyo wa watu 116 kwa kilometa mraba[1].

Mji mkuu uko Kilifi lakini mji mkubwa zaidi ni Malindi.

Kiongozi wa serikali yake ni gavana anayechaguliwa na wananchi.

Eneo la kaunti liko upande wa kaskazini na kaskazini-mashariki ya Mombasa. Sehemu zinazotembelewa na watalii ni hasa Kikambala, Watamu, Malindi na Kilifi.

  1. www.knbs.or.ke

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search