Kenya

Jamhuri ya Kenya (Kiswahili)
Bendera ya Kenya Nembo ya Kenya
(Bendera ya Kenya) (Nembo ya Kenya)
Lugha rasmi Kiswahili, Kiingereza
Mji Mkuu Nairobi
Mji Mkubwa Nairobi
Miji mingine Mombasa, Kisumu na Nakuru
Serikali Jamhuri
Rais William Ruto
Eneo km² 580,367
Idadi ya wakazi 47,564,296 (2019)
Wakazi kwa km² 82
Jumla la pato la taifa kinaganaga Bilioni $114.68[1]
Jumla la pato la taifa kwa kila mtu $2,252[1]
Pesa Shilingi ya Kenya
Kaulimbiu "Harambee"
Wimbo wa Taifa Ee Mungu Nguvu Yetu
Kenya katika Afrika
Saa za Eneo UTC +3 (Wakati wa Afrika Mashariki)
Mtandao .ke
Kodi ya Simu +254

Jamhuri ya Kenya ni nchi iliyoko Afrika Mashariki katika ikweta, kando ya Bahari ya Hindi.

Kenya imepakana na Ethiopia (kaskazini), Somalia (kaskazini mashariki), Tanzania (kusini), Uganda na Ziwa Victoria (magharibi), kisha Sudan Kusini (kaskazini magharibi).

Kenya ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na wa miundo mingine mbalimbali ya kimataifa.

Mji mkuu ni Nairobi.

Idadi ya watu imeongezeka sana katika miaka ya karibuni na kufikia milioni 49.

Kenya ina mbuga mbalimbali wanamoishi aina elfu kadhaa za wanyama pori.

Jina la nchi limetokana na mlima Kenya[2], ulio wa pili kwa urefu barani Afrika.[3][4]

  1. 1.0 1.1 "World Economic Outlook database: April 2022". imf.org.
  2. Kabla ya mwaka wa 1920, eneo linaloitwa Kenya liliitwa Himaya ya Uingereza Afrika Mashariki, kwa hiyo hapakuwa na haja ya kutaja neno mlima uliporejelea mlima huo.
  3. The Times|articlename=British East Africa Annexed--"Kenya Colony" |author=Reuter|section=News|day_of_week=Thursday|date=8 Julai 1920|page_number=13|issue=42457|column=C
  4. "East Africa: Kenya: History: Kenya Colony". Encyclopedia Britannica. 17 (15 ed.). 2002. pp. 801, 1b. ISBN 0-85229-787-4.

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search