Kidagba

Kidagba ni lugha ya Kinilo-Sahara nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na Chad inayozungumzwa na Wadagba. Mwaka wa 2007 idadi ya wasemaji wa Kidagba nchini Afrika ya Kati imehesabiwa kuwa watu 34,000. Pia kuna wasemaji 10,000 nchini Chad. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kidagba iko katika kundi la Kibongo-Bagirmi.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search