Kigbanziri

Kigbanziri ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati inayozungumzwa na Wagbanziri. Mwaka wa 1996 idadi ya wasemaji wa Kigbanziri nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati imehesabiwa kuwa watu 14,500. Pia kuna wasemaji 3000 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kigbanziri iko katika kundi la Kiadamawa-Ubangi.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search