Kilangbashe

Kilangbashe ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inayozungumzwa na Walangbashe. Wataalamu wengine huiangalia kuwa lahaja ya Kibanda ya Kusini. Mwaka wa 1996 idadi ya wasemaji wa Kilangbashe nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati imehesabiwa kuwa watu 40,000. Pia kuna wasemaji 3000 nchini Kongo. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kilangbashe iko katika kundi la Kiadamawa-Ubangi.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search