Kimalagasy

Kimalagasy

Kimalagasy ni mlolongo wa lugha za Kiaustronesia nchini Madagaska inayozungumzwa na Wamalagasy. Lugha za Kimalagasy hasa ni Kiantankarana, Kibara, Kibetsimisaraka-Kaskazini, Kibetsimisaraka-Kusini, Kimasikoro, Kisakalava, Kimalagasy Sanifu, Kitandroy-Mahafaly, Kitanosy, Kitesaka na Kitsimihety. Idadi ya wasemaji wote wa lugha za Kimalagasy imezidi watu milioni 16. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, lugha za Kimalagasy iko katika kundi la Kibarito.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search