Kirundi

Kirundi ni lugha ya Kibantu inayotumika na watu milioni kumi au zaidi hasa nchini Burundi lakini pia katika maeneo ya jirani ya Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Uganda. Ndiyo lugha ya taifa na mojawapo ya lugha rasmi za Burundi.

Wanaosema Kirundi na Kinyarwanda, lugha rasmi ya Rwanda, wanasikilizana bila shida.[1]

Kwa kiasi kikubwa sana hata Waha na Wahangaza wa Tanzania wanasikilizana nao.

  1. Ethnologue, 15th ed.

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search