Kisimbiti (au Kisuba-Kisimbiti) ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wasimbiti, Wahacha, Wakine, Wasweta, Wasurwa na Waroba. Pia huitwa Kisuba-Kisimbiti. Lahaja zake ni pamoja na Kihacha, Kisweta na Kisurwa. Lugha ya Kisuba-Kisimbiti isichanganywe na lugha ya Kisuba nchini Kenya.
Mwaka wa 2011 idadi ya wasemaji wa Kisimbiti imehesabiwa kuwa watu 113,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kisimbiti iko katika kundi la E40.
© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search