Kiyaka (Afrika ya Kati)

Kiyaka ni lugha ya Kibantu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na Jamhuri ya Kongo inayozungumzwa na Wayaka. Isichanganywe na lugha ya Kiyaka nchini Jamhuri ya Kongo wala na lugha ya Kiyaka nchini Angola. Mwaka wa 1996 idadi ya wasemaji wa Kiyaka nchini Afrika ya Kati imehesabiwa kuwa watu 15,000. Pia kuna wasemaji 15,000 tena nchini Kongo. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kiyaka iko katika kundi la C10.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search