| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Taifa moja, Lengo moja, Imani moja (Kifaransa: Un peuple, un but, une foi) | |||||
Wimbo wa taifa: Pour l'Afrique et pour toi, Mali (Kwa Afrika na kwako, Mali) | |||||
![]() | |||||
Mji mkuu | Bamako | ||||
Mji mkubwa nchini | Bamako | ||||
Lugha rasmi | Kibambara na nyingine 12[1] | ||||
Serikali | Jamhuri Assimi Goïta Choguel Kokalla Maïga | ||||
Uhuru Tarehe |
kutoka Ufaransa 22 Septemba 1960 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
1,240,192 km² (ya 23) 1.6% | ||||
Idadi ya watu - 2022 kadirio - 2018 sensa - Msongamano wa watu |
21,473,764 (ya 60) 19,329,841 11.7/km² (ya 215) | ||||
Fedha | CFA franc (XOF )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC0) (UTC+1) | ||||
Intaneti TLD | .ml | ||||
Kodi ya simu | +223
- |
Mali, rasmi jamhuri ya Mali, ni nchi isiyo na pwani katika Afrika Magharibi, ikiwa na mpaka na Algeria, Niger, Burkina Faso, Kodivaa, Guinea, Senegal, na Mauritania. Mji mkuu wake na mji mkubwa zaidi, Bamako, ni kitovu cha kiutamaduni na kiuchumi wa nchi hiyo. Kwa idadi ya watu takriban milioni 21.9 (makadirio ya 2023), Mali iko katika nafasi ya 59 kwa watu duniani. Nchi hiyo inajulikana kwa umuhimu wake wa kihistoria kama kitovu cha Milki ya Mali na mji wa kihistoria wa Timbuktu, ambayo ilikuwa kitovu cha kielimu na biashara wakati wa enzi za kati.
Sehemu ya juu ni mlima Hombori Tondo (mita 1155 juu ya UB) ulioko katikati ya nchi.
Upande wa Kaskazini sehemu kubwa ya eneo la Mali ni jangwa la Sahara.
Wakazi walio wengi huishi kusini, karibu na mito Senegal na Niger.
© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search