Mchungaji

Mchungaji na kundi lake, mchoro wa mwaka 1905 hivi.
Kristo akimuagiza Petro kadiri ya Raphael, 1515.
Mchungaji wa Kimethodisti katika mavazi yake rasmi.

Mchungaji ni mtu anayechunga mifugo, kama vile kondoo, lakini pia watu, hasa katika Ukristo, ambapo ni cheo maalumu katika madhehebu ya Uprotestanti.

Kihistoria, uchungaji ulianza katika Mashariki ya Kati miaka 5,000 hivi iliyopita.

Katika Biblia kazi hiyo ilitumika sana kufafanua majukumu ya wafalme na viongozi wengine. Daudi alichukuliwa kama kielelezo.

Manabii walitabiri ujio wa mwana wa Daudi atakayechunga vizuri taifa la Israeli kwa niaba ya Mungu.

Yesu alijitambulisha kama mchungaji mwema aliye tayari kutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo zake (Yoh 10:11).

Mwenyewe alimkabidhi Mtume Petro uchungaji wa kundi lake (Yoh 21:16).

Mfano huo unatumika pia kwa watu wengine (Mdo 20:17,28; 1Kor 9:7; Ef 4:11; 1Pet 5:12).

Katika ibada Maaskofu wa Kanisa Katoliki na wengineo wanatumia bakora kujitambulisha kama wachungaji.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search