| |||||
Kaulimbiu ya taifa: (hakuna) | |||||
Wimbo wa taifa: Himno Nacional Mexicano | |||||
![]() | |||||
Mji mkuu | Mji wa Mexiko (Kihisp.: Ciudad de Mexico) | ||||
Mji mkubwa nchini | Mji wa Mexiko (Kihisp.: Ciudad de Mexico) | ||||
Lugha rasmi | (hakuna kitaifa) Kihispania (hali halisi) | ||||
Serikali | Shirikisho la Jamhuri Claudia Sheinbaum | ||||
Uhuru Imetangazwa imetambuliwa |
16 Septemba 1810 27 Septemba 1821 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
1,972,550 km² (ya 15) 2.5% | ||||
Idadi ya watu - 2023 kadirio - 2000 sensa - Msongamano wa watu |
129,875,529 (ya 10) 101,879,171 61/km² (ya 142) | ||||
Fedha | Peso (MXN )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-8 to -6) varies (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .mx | ||||
Kodi ya simu | +52
- |
Meksiko (jina rasmi: Mataifa ya Muungano wa Mexico) ni nchi kubwa (km2 1,972,550) inayohesabiwa kijiografia kuwa sehemu ya Amerika ya Kaskazini au pengine ya Amerika ya Kati. Kwa vyovyote kiutamaduni ni sehemu ya Amerika ya Kilatini.
Imepakana na Marekani upande wa kaskazini. Upande wa kusini-mashariki majirani ni Guatemala na Belize.
Ina pwani ndefu kwenye bahari za Pasifiki upande wa magharibi na kusini na Ghuba ya Meksiko na Bahari ya Karibi upande wa mashariki.
Ina muundo wa jamhuri ya shirikisho ya majimbo 32 yanayojitawala, yenye idadi ya watu takriban milioni 129, na kuifanya kuwa nchi ya 10 yenye idadi kubwa ya watu duniani.
Meksiko ilikuwa nchi ya staarabu za juu ya Waazteki na Wamaya hadi kuvamiwa na Hispania mnamo mwaka 1521, halafu koloni la Hispania hadi uhuru wa mwaka 1821.
Kwa sasa ni nchi ya 15 kiuchumi duniani, hivyo ni pia mwanachama wa kundi la G20.
Mji mkuu ni Mexico City, ambao katika eneo lake lote una watu zaidi ya milioni 20, hivyo ni mojawapo ya maeneo ya mijini yenye watu wengi zaidi duniani.
© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search