Milima ya Zagros

Maeneo ya milima ya Zagros nchini Iran (mstari mwekundu)
Mlima Dena, kilele cha juu katika milima ya Zagros.

Milima ya Zagros (kwa Kifarsi: کوه‌های زاگرس kuh-haye zagros) ni safu ya milima katika magharibi na kusini-magharibi nchini Iran ikienea pia katika Iraki na Uturuki.

Urefu wake ni mnamo kilomita 1,500. Safu inaanza kaskazini-magharibi mwa Iran, ikifuata mpaka wa magharibi wa nchi hiyo halafu pwani ya Ghuba ya Uajemi upande wa kusini, ikiishia kwenye mlangobahari wa Hormuz.

Miinuko ya juu zaidi katika Milima ya Zagros ni Zard Kuh (mita 4,548) na mlima Dena (m 4,359).

Eneo la Zagros ni sehemu muhimu ya uzalishaji wa mafuta ya petroli.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search