Mombasa | |
---|---|
Jiji | |
![]() |
|
Nchi | ![]() |
Jimbo | Kaunti ya Mombasa |
Serikali | |
Gavana | Abdulsamad Shariff Nassir |
Utaifa | M-Mombasa (en: Mombasan) |
Eneo | |
Jumla | 219.9 km² |
Idadi ya watu | |
Jumla | 1,208,333 |
Msongamano | 5,495/km²/km² |
Pato la Taifa | |
Jumla (2022) | $13.132 bilioni |
HDI (2023) | 0.699 (2) |
Eneo la saa | UTC+3 (EAT) |
Tovuti: mombasa.go.ke |
Mombasa ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Kenya katika eneo la Pwani ya Kenya.Mombasa ni bandari muhimu Afrika Mashariki na ndio kubwa zaidi eneo la Afrika ya Mashariki. Mji huu uko kwenye mwambao wa Bahari Hindi.Mnamo 2019 ulikuwa na idadi ya watu takriban milioni 1.2 na eneo la kilomita za mraba 219.9
Baada ya kuundwa kwa serikali ya ugatuzi, Mombasa umekuwa mji mkuu wa kaunti ya Mombasa.
Mombasa ni kitovu cha utalii wa pwani ya Kenya. Watalii wengi hufika kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Moi. Wengine pia husafiri kupitia barabara kutoka Nairobi wakitazama mandhari mbalimbali. Kutoka Nairobi kwenda Mombasa ni takribani kilomita 483.77. Watalii wengi hupenda kuuona mji wa Mombasa kwanza, kisha wanaunganisha ndege hadi Kilimanjaro na sehemu nyingine zilizo na vivutio nchini Tanzania.
Kati ya ishara ya mji ni Boma la Yesu na pembe za Mombasa.
Kiswahili cha Mombasa huitwa Kimvita.
Mombasa na Seattle ni "miji-ndugu".
© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search