Mtaguso wa Trento

Mtaguso ukifanyika katika kanisa kuu la Trento.

Mtaguso wa Trento (uliofanyika kwa kwikwi kuanzia mwaka 1545 hadi 1563), unahesabiwa na Kanisa Katoliki kuwa mtaguso mkuu wa kumi na tisa.

Miaka hiyo maaskofu wa Kanisa Katoliki walikutana Trento, Italia Kaskazini, wakajadiliana juu ya mafundisho na hali ya Kanisa, wakachukua hatua za kuimarisha imani na kuondoa matatizo.

Huo Mtaguso, ulioitishwa kizazi kimoja baada ya matengenezo ya Martin Luther, ulianza kabla ya vita vya Schmalkald (1546-1547) ukamalizika baada ya amani ya Augsburg (1555).

Mwishoni mwa kikao cha tatu ilionekana wazi kuwa umoja wa Kanisa la magharibi umekwisha. Haikuwezekana kufuta farakano lililotokea tayari.

Mtaguso huo, uliochukua muda mrefu kuliko yote ya historia, ulieneza urekebisho wa Kanisa na kuchukua msimamo kuhusu mafundisho ya Waprotestanti waliojitokeza katika hiyo karne ya 16.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search