Mtaguso wa tano wa Laterano

Bulla monitorii et declarationis
Litterae super abrogatione pragmatice sanctionis, 1512

Mtaguso wa tano wa Laterano ulifanyika kuanzia mwaka 1512 hadi 1517 huko Roma (Italia), kwenye Basilika la Mt. Yohane huko Laterano ambalo ndilo kanisa kuu la Jimbo Katoliki la Roma.

Kanisa Katoliki linauhesabu kama mtaguso mkuu wa kumi na nane.

Uliitishwa na Papa Julius II (1503-1513) ambaye alianza kuusimamia tarehe 3 Mei 1512. Baada ya kifo chake, uliendelezwa na Papa Leo X (1513-1521) hadi kikao cha 12 na cha mwisho kilichofanyika tarehe 16 Machi 1517.

Ulihudhuriwa na maaskofu 100 hivi, wengi wao wakitokea Italia. Kutofika kwa wajumbe kutoka nchi nyingine, pamoja na wengi kukosa nia ya kujirekebisha, kulichangia kufanya utekelezaji wa maamuzi ya mtaguso ushindikane.

Maamuzi hayo yalitolewa kwa hati za Papa. Mengine yanahusu mafundisho ya imani, mengine maagizo ya urekebisho wa Kanisa.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search