Muujiza

Mchoro wa mwaka 1410 hivi kutoka Très Riches Heures du Duc de Berry, Musée Condé, Ufaransa ukitaka kuonyesha Ufufuko wa Lazaro uliotokea siku nne baada ya kifo chake, muujiza mkuu uliofanywa na Yesu Kristo.

Muujiza ni tukio lisiloelezeka kisayansi kufuatana na sheria za maumbile.[1]

Matukio hayo yanaweza kufikiriwa yamesababishwa ama na Mungu au miungu, hata kupitia mtu wa dini, ama na nguvu nyingine zinazohusiana na ushirikina.

Hayo ni tofauti kabisa na matukio ambayo yanapatikana kwa nadra lakini yanaweza kuelezwa kisayansi ambayo watu wengine wakiyashangaa na kuyafurahia wanayaita miujiza.

  1. "Miracle". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-09-02. Iliwekwa mnamo 2016-03-25.

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search