Mzizi

Kwa matumizi mengine ya jina hili angalia Mizizi

Mzizi katika isimu ni sehemu muhimu sana ya neno ambayo haibadiliki hata kama neno litafanyiwa uambishaji, ukanushi, unyambulishaji na kadhalika. Sehemu hii ikibadilika, hata dhana ya neno hilo hubadilika

Mzizi wa neno ni sehemu ya neno inayobaki baada ya kuondoa viambishi tamati na viambishi awali au, kwa maneno mengine, mzizi wa neno ni sehemu yake inayobaki baada ya kuondoa viambishi vyote.

Kwa mfano: mzizi wa neno "Analima" ni "lim". Hii hutokana na kuchukua neno na kisha kulitafutia shina lake (kitenzi) na kisha kuondoa kiambishi tamati "a".


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search