Nyandira

Nyandira ni mojawapo ya kata zilizopo katika wilaya ya Mvomero, mkoa wa Morogoro, Tanzania yenye Postikodi namba 67323.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 7,801 [1].

Katika kata hii wakazi walio wengi ni Waluguru. Upande wa dini, wengi wao ni Wakristo wa Kanisa Katoliki.

Wakazi wa eneo hili wanashughulika zaidi na kilimo, biashara, ufugaji na elimu. Zaidi sana wakazi wa kata hii wanashughulika na masuala ya utamaduni, kwa mfano, ngoma za asili kama vile mbeta, chikudindi, ritutu, chibwiko n.k.

Kata hii ina vijiji na vitongoji mbalimbali, vikiwemo: Chogo, Mtamba, Mhvisomi, Magana, Lubwe,kibuko Vidigisi, Ndughutu, Msewe, Tawa.

  1. https://www.nbs.go.tz

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search