Nyumba

Nyumba ya Kasbah nchini Moroko hujengwa kwa udongo ulioshindiliwa

Nyumba ni jengo lenye shabaha ya kuwapa watu makazi na nafasi ya kuishi humo. Watu walianza kujenga nyumba tangu miaka mielfu mingi kama kinga dhidi ya hali ya hewa na athari za jua, usimbishaji au baridi. Nyumba ni makazi ya kudumu tofauti na makazi ya muda kama hema.

Kuna nyumba ndogo yenye chumba kimoja tu lakini kuna pia nyumba zenye vyumba mamia. Pale ambako nafasi ya kujenga ni haba kuna nyumba za ghorofa. Kiasili maghorofa yalijengwa pia kwa sababu za usalama.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search