Plau

Trekta inavuta plau yenye ulimi 5; ardhi nyuma ya plau imegeuzwa
Plau sahili huko Misri mnamo 1200 KK; aina hii bado inatumiwa katika nchi kadhaa

Plau (kut. Kiing. plough (UK) au plow (US)) ni mashine sahili ya kulimia ardhi kwenye kilimo.

Plau huvutwa shambani kwa nguvu ya trekta au mashine, mnyama au pia ya kibinadamu. Ulimi wa plau unakata ardhi na kuigeuza. Kwa njia hii ardhi inalainishwa na tabaka za chini zenye lishe mpya ya mimea zinapelekwa juu. Vilevile majani yasiyotakiwa yanachimbwa chini ya ardhi hivyo kuipa nafasi mimea mipya kutokana na mbegu unaopandwa.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search