Sheria za Kanisa

Kurasa za Decretum ya Burchard wa Worms, kitabu cha sheria za Kanisa cha karne ya 11.

Sheria za Kanisa ni taratibu zilizokubaliwa na mamlaka ya Kanisa katika kuendesha shughuli zake za ndani na za nje. Awali sheria za namna hiyo zilitolewa na Mitume wa Yesu, halafu na waandamizi wao, hasa maaskofu waliokusanyika katika mitaguso na sinodi mbalimbali[1]

Umuhimu wa sheria hizo ni tofauti kadiri ya madhehebu husika.

Katika karne ya 20 Kanisa Katoliki, maarufu kwa kutia maanani umoja na utaratibu, limekusanya sheria zake muhimu zaidi katika vitabu viwili vya Kilatini: kimoja kwa Kanisa la Kilatini (Codex Iuris Canonici), kingine kwa Makanisa Katoliki ya Mashariki (Codex Canonum Ecclesiarium Orientalium).

  1. Boudinhon, Auguste. "Canon Law." The Catholic Encyclopedia. Vol. 9. New York: Robert Appleton Company, 1910. 9 Aug. 2013

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search