Shilingi ya Kenya

sarafu ya KSh 10

Shilingi ya Kenya (KES au Ksh) ni fedha za Kenya. Shilingi moja imegawanywa kwenye senti mia moja.

Shilingi ya Kenya ilianzishwa mwaka 1966 baada ya kuvunjwa kwa bodi ya fedha ya Afrika ya Mashariki iliyosimamia fedha ya pamoja ya Kenya, Tanzania na Uganda iliyoitwa East African Shilling iliyotumiwa katika maeneo yote yaliyokuwa chini ya Uingereza katika Afrika ya Mashariki.

Kuna sarafu za shilingi 1, 5, 10, 20 na 40.

Sarafu za senti zipo za zamani za senti 1, 5, 10, 20 na 50 lakini hazinunui kitu tena.

Noti zilitolewa za shilingi 5, 10, 20, 50, 100, 200, 500 na 1000 ingawaje noti za shilingi 5, 10 na 20 ni nadra sana kuonekana.

  • Shilingi 1 = Senti 100

Majina ya zamani:

  • Thumuni 1 = Senti 50
  • Peni 1 = Senti 10
  • Ndururu 1 = Senti 5

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search