الإسلام (Al-Islām) | |
Uainishaji | ya Ibrahimu |
Maandiko | Qur'an Hadith |
Teolojia | Mungu mmoja (Allah) |
Eneo | Duniani kote, hasa Mashariki ya Kati, Asia ya Kusini, Afrika Kaskazini |
Lugha | Kiarabu cha Qur'an |
Mwaasisi | Mtume Muhammad |
Asili | Karne ya 7 BK, Arabia |
Ibada | Sala, Saumu, Zaka, Hija, Shahada |
Wafuasi | Bilioni 1.9[1] |
Uislamu (kwa Kiarabu: الإسلام Al-Islām) ni dini inayotokana na mafunzo ya Mtume Muhammad. Wafuasi wa imani hiyo huitwa "Waislamu" na wanakadiriwa kuwa milioni 1,800 hivi. Hivyo ni dini ya pili duniani yenye wafuasi wengi baada ya Ukristo wenye wafuasi milioni 2,400.
Uislamu ni ile imani kuwa muumba ni mmoja tu kwa dhati na sifa zake. Nguzo nyingine za imani zinajengwa juu ya imani ya Mungu mmoja wa kweli, imani juu ya maisha baada ya kifo, imani juu ya Malaika wa Mungu, vitabu vyake na kudra na tafsiri ya vitendo ya imani hii ni: Sala, Zakah, Saumu na Hija.
© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search