Usiku

Dunia wakati wa usiku; picha hii imeunganishwa kutokana na picha mbalimbali zilizopigwa na chomboanga. Hali halisi hakuna eneo lote linaloonekana liko gizani wakati mmoja. Nukta nyeupe upande wa kulia ni nuru ya miji wakati wa giza.
Kutwa huko Albuquerque, New Mexico.

Usiku ni kipindi cha siku kilichopo kati ya machweo na macheo na hasahasa kipindi cha giza kinachotokea baada ya machweo ambapo mwanga wa jua hauonekani tena angani hadi muda mfupi kabla ya macheo yaani kabla ya jua kuonekana juu ya upeo wa anga.

Kinyume chake ni mchana.

Kutokana na kupoteapotea kwa nuru ya jua, nyota zinaonekana usiku (pasipo mawingu).

Watu wengi pamoja na wanyama wengi hulala usiku, lakini kuna wanyama wengine wanaofanya shughuli zao usiku kama vile bundi, popo na wadudu wengi.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search