Wakartusi

Badge of the Carthusian Order
Monasteri ya zamani huko Seville, Hispania.
Ramani ya nyumba ya Kikartusi ya kawaida (Clermont), iliyochorwa na Eugène Viollet-le-Duc mwaka 1856.
Jinsi Francisco de Zurbarán alivyomchora askofu Hugo wa Grenoble akitembelea Kartusi.

Shirika la Wakartusi, au Shirika la Mt. Bruno, ni utawa mmojawapo wa Kanisa Katoliki. Wamonaki wake wote, wanaume kwa wanawake wanaishi ndani kwa ndani: wengine katika nyumba za binafsi, wengine katika makao ya pamoja.

Shirika lilianzishwa na Bruno Mkartusi mwaka 1084.

Linafuata sheria zake, badala ya kanuni ya Benedikto wa Nursia inayoongoza wamonaki karibu wote wa Kanisa la Kilatini.

Jina linatokana na milima ya Chartreuse (nchini Ufaransa), ambapo Bruno na wakaapweke wenzake 6 walijenga makao ya kwanza.

Kaulimbiu ya shirika ni: Stat crux dum volvitur orbis (kwa Kilatini "Msalaba unadumu wakati ulimwengu unabadilikabadilika."


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search